Wikiversity
Yaliyomo
Ramani ni picha - kwa kawaida mchoro - ya dunia au sehemu au sifa zake.
Ni tofauti na picha iliyopigwa kwa kamera kutoka ndege au chombo cha angani kwa sababu mchora ramani anachagua anachotaka kuonyesha na kuzipa uzito sifa anazotaka kuziwekea mkazo.
Kuna aina nyingi za ramani:
- ramani za topografia huonyesha sura ya nchi (kwa mfano: bahari, nchi kavu, milima, mito, kimo cha ardhi na kina cha bahari)
- ramani za idadi huonyesha sifa fulani kuhusiana na dunia (kwa mfano: historia, uchumi, mtawanyiko wa wakazi katika nchi n.k.)
- ramani inaweza kufuata sura ya nchi
- ramani inaweza kufuata mahitaji ya msomaji (ramani ya njia ya reli huonyesha mstari tu na mfuatano wa vituo bila kutaja kona na mabadiliko ya mwelekeo)
Kila mchoraramani anahitaji kuchagua jinsi ya kuonyesha mambo yake. Kwa ramani za kijiografia tatizo hutokana na umbo la dunia ambalo ni tufe wakati ramani kwa kawaida ni karatasi bapa.
Viungo vya nje
- International Cartographic Association (ICA)
- Mwongozo wa Jiografia na Ramani.
- The History of Cartography Project
- Mapping History Project - Chuo Kikuu cha Oregon