Wikiversity
Yaliyomo
Popo | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Popo-masikio wa Townsend
(Corynorhinus townsendii) | ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Nusuoda 2:
|
Popo ni mamalia kama panya wenye mabawa.
Spishi zake nyingi sana hula wadudu: hizi zimo katika nusuoda Yangochiroptera.
Spishi kubwa za nusuoda hii hula ndege, mijusi, vyura na hata samaki.
Spishi chache za popo wanyonya-damu huko Amerika ya Kusini hula damu ya mamalia au ndege.
Familia Pteropodidae ya nusuoda Yinpterochiroptera ina spishi kubwa hadi ukubwa wa paka na uzito wa kilogramu moja; urefu wa mabawa pamoja unaweza kufikia sentimita 150. Spishi hizi hula matunda.
Uainishaji
Hapo awali, popo waligawanywa katika nusuoda Microchiroptera na Megachiroptera. Walakini, tafiti za ADN zilifunua kuwa baadhi ya familia za Microchiroptera zilikuwa karibu na Megachiroptera. Kwa hivyo, nusuoda mbili mpya zilipendekezwa, Yangochiroptera na Yinpterochiroptera. Nusuoda ya mwisho imegawanywa katika familia za juu Pteropodoidea (popo-matunda) na Rhinolophoidea (popo-wadudu; spishi mbalimbali hula vertebrata wadogo).
Utambuaji kwa mwangwi
Popo wengi hutumia sauti kwa kutambua mazingira yao, yaani wanatumia mwangwi wa mlio wao kukadiria umbali hadi kizuizi au hata windo pamoja na ukubwa na maumbile ya vitu vilivyopo njiani. Kwa hiyo masikio yao ni mlango wa fahamu muhimu zaidi. Kinyume chake popo wengi hawana macho mazima ingawa hakuna aliye kipofu kabisa. Lakini kuna pia aina nyingine wanaoona vizuri sana.
Picha
-
Popo-matunda (pande)
-
Popo-wadudu (popo-njumu)
-
Masikio ni mlango wa fahamu muhimu zaidi kuliko macho