Wikiversity
Mwezi wa Juni ni mwezi wa sita katika Kalenda ya Gregori. Jina lake limetokana na jina la mungu wa Warumi Juno.
Tarehe 21 ya mwezi huo wa Juni (katika miaka mingine inawezekana kuwa tarehe 20 au 22) ni siku ya solistasi ya Kaskazini (kutoka Kiingereza solstice), yaani wakati jua linapokuwa kaskazini kabisa mwa Ikweta.
Juni ina siku 30, na hakuna mwezi mwingine unaoanza na siku ya juma sawa na mwezi wa Juni katika mwaka uleule.