LIMSwiki
Yaliyomo
Sanamu ni kazi ya sanaa ambayo inatofautiana na picha au mchoro kwa sababu inaonyesha mtu au kitu si kwa urefu na upana, bali pia kwa unene.
Inaweza kutengenezwa kwa kuchonga au kwa njia nyingine (k.mf. kumimina kiowevu katika muundo uliokusudiwa).
Historia
Sanamu zilitengenezwa tangu zamani za historia ya awali (walau miaka 30,000 hivi iliyopita) na katika utamaduni mbalimbali wa dunia nzima. Ile ndefu zaidi ni sanamu ya Buddha inayopatikana China ikiwa na urefu wa mita 128.
Mara nyingi sanamu inaagizwa kama kumbukumbu ya tukio fulani au mtu maarufu na inawekwa mahali pa hadhara.
Katika dini
Dini mbalimbali, hasa Uyahudi na Uislamu, zimekataza sanamu na picha zote.
Katika Ukristo suala lilijadiliwa kwa nguvu zote hasa katika karne ya 7 na ya 8 likamalizika katika mtaguso wa pili wa Nisea. Hata hivyo, baadaye lilizuka tena na tena, hivi kwamba msimamo wa madhehebu ni tofauti sana.
Picha
-
Simba-mtu, Hohlenstein-Stadel, Ujerumani, sasa katika Ulmer Museum, Ulm, ni sanamu ya kale kuliko zote zinazojulikana kuonyesha kiumbehai, 40,000 - 30,000 KK
-
Mungu jike Venus wa Dolní Věstonice, 29,000 - 25,000 KK
-
Venus wa Willendorf, 24,000 - 22,000 KK
-
Great Sphinx wa Giza (Misri), 2558 – 2532 KK, sanamu kutoka mwamba mmoja iliyo kubwa kuliko zote duniani (mita 73.5 x 6 x 20.22)
-
Hermes na mtoto Dionysus, kazi ya Praxiteles, Karne ya 4 KK, Archaeological Museum of Olympia, Ugiriki
-
Spring Temple Buddha, sanamu yenye kimo kirefu kuliko zote duniani, ilimalizika 2002, China
Tanbihi
Viungo vya nje
- UK Public Monument and Sculpture Association Ilihifadhiwa 17 Februari 2007 kwenye Wayback Machine.