LIMSwiki

Alternative text
Reuters London

Reuters ni shirika la habari linalomilikiwa na Thomas Reuters[1] Ni kati ya vyombo vya habari vikubwa na vinavyoaminiwa sana ulimwenguni.[2]

Shirika hili limeajiri waandishi wa habari takriban 2500 na wapiga picha habari wapatao 600 waliosambazwa kwenye vituo 200 katika maeneo mbalimbali ya dunia na kuripoti katika lugha 16 tofauti.[3]

Shirika hili liliasisiwa jijini London mnamo mwaka 1851 na mtu mwenye asili ya Ujerumani, Paul Reuters. Baadaye lilinunuliwa na Thomson Corporation ya Canada mnamo mwaka 2008 na sasa limekuwa tawi linaloshughulika na habari la kampeni kuu ya Thomson Reuters.[4]

Tanbihi

  1. "Thomson Reuters | History & Facts | Britannica.com". web.archive.org. 2018-11-07. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-07. Iliwekwa mnamo 2024-10-09.{{cite web}}: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)
  2. Reuters
  3. Reuters
  4. Stephen Brook (30 Mei 2006). "Reuters recruits 100 journalists". The Guardian. Iliwekwa mnamo 5 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)