LIMSwiki

Papa Klementi XI.

Papa Klementi XI (23 Julai 164919 Machi 1721) alikuwa Papa kuanzia tarehe 23/30 Novemba/8 Desemba 1700 hadi kifo chake[1]. Alitokea Urbino, Italia[2].

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Giovanni Francesco Albani.

Alimfuata Papa Inosenti XII akafuatwa na Papa Inosenti XIII.

Tazama pia

Sala maarufu iliyosambazwa kwa jina lake

Nasadiki, Bwana, lakini nisadiki kwa imara zaidi; natumaini, lakini nitumaini kwa hakika zaidi; napenda, lakini nipende kwa ari zaidi; nasikitika, lakini nisikitike kwa nguvu zaidi.

Nakuabudu kama asili ya vyote; nakutamani kama lengo kuu; nakusifu kama mfadhili wa kudumu; nakulilia kama mtetezi wa kufaa.

Uniongoze kwa hekima yako, unidhibiti kwa haki yako, unifariji kwa wema wako, unilinde kwa uwezo wako.

Bwana, nakutolea ya kuwaza ili yakuelekee wewe, ya kusema yakuhusu wewe, ya kufanya yawe kadiri yako, ya kuvumilia yake kwa ajili yako.

Nataka chochote unachotaka, nataka kwa sababu unataka, nataka jinsi unavyotaka, nataka mpaka utakapotaka.

Naomba, Bwana: angaza akili, washa utashi, safisha moyo, takasa roho.

Nilie juu ya maovu yaliyopita, nifukuze vishawishi vijavyo, nirekebishe maelekeo mabaya, nistawishe maadili ya kufaa.

Mungu mwema, unipatie upendo kwako, chuki kwangu, ari kwa jirani, dharau kwa ulimwengu.

Nijitahidi kutii wakubwa, kusaidia walio chini yangu, nishauri marafiki, nisamehe maadui.

Nishinde tamaa kwa maisha magumu, uroho kwa ukarimu, hasira kwa upole, uvuguvugu kwa umotomoto.

Unifanye niwe na busara katika maamuzi, niwe na msimamo katika hatari, niwe mvumilivu katika matatizo, na mnyenyekevu katika mafanikio.

Ee Bwana, fanya niwe mwangalifu katika sala, niwe na kiasi katika mali, niwe na bidii katika majukumu, niwe imara katika nia.

Nijitahidi kuwa na usafi wa ndani, utaratibu wa nje, maongezi bora, maisha yanayofuata mipango.

Nikeshe kwa bidii kutawala umbile, kustawisha neema, kufuata sheria, kustahili wokovu.

Nijifunze kwako yalivyo duni mambo ya dunia, yalivyo makuu mambo ya Kimungu, yalivyo mafupi mambo yapitayo, yanavyodumu yale ya milele.

Unijalie nijiandae kwa kifo, niogope hukumu, nikimbie moto, nipate paradiso.

Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Klementi XI kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa .