LIMSwiki
Yaliyomo
Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.
Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini[1].
Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.
Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio,pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili[2]
Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya[3]. Kinga ni bora kuliko tiba.
Tazama pia
Tanbihi
- ↑ "How vaccines work | British Society for Immunology". www.immunology.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-31.
- ↑ Raphael Hans. "Fact and truth about covid vaccine" (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-12. Iliwekwa mnamo 2021-03-31.
- ↑ "Vaccines and immunization". www.who.int (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-31.
Viungo vya nje
- Vaccines and Antisera katika Open Directory Project
- WHO Vaccine preventable diseases and immunization
- World Health Organization position papers on vaccines
- The History of Vaccines, from the College of Physicians of Philadelphia
- University of Oxford Vaccinology Programme: a series of short courses in vaccinology Archived 11 Aprili 2016 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chanjo kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa . |