LIMSwiki
Yaliyomo
Mandhari
Tarehe 9 Julai ni siku ya 190 ya mwaka (ya 191 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 175.
Matukio
Waliozaliwa
- 1249 - Kameyama, mfalme mkuu wa Japani (1259-1274)
- 1578 - Kaisari Ferdinand II wa Ujerumani
- 1654 - Reigen, Mfalme Mkuu wa Japani (1663-1687)
- 1887 - Samuel Eliot Morison, mwandishi na mwanahistoria kutoka Marekani
- 1926 - Ben Mottelson, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1975
- 1956 - Tom Hanks, mwigizaji kutoka Marekani
Waliofariki
- 1572 - Watakatifu Wafiadini wa Gorkum nchini Uholanzi
- 1727 - Mtakatifu Veronika Giuliani, bikira mmonaki wa Waklara Wakapuchini nchini Italia
- 1850 - Zachary Taylor, Rais wa Marekani (1849-1850)
- 1900 - Mtakatifu Fransisko Fogolla, O.F.M., askofu Mkatoliki kutoka Italia na mfiadini nchini Uchina
- 1900 - Mtakatifu Amadina, bikira Mfransisko kutoka Ubelgiji na mfiadini nchini Uchina
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Augustino Zhao Rong na wenzake, Nikola Pieck na wenzake, Veronika Giuliani, Yohakimu He Kaizhi, Paulina Visintainer n.k.