LIMSwiki
Yaliyomo
Mandhari
Tarehe 3 Oktoba ni siku ya 276 ya mwaka (ya 277 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 89.
Matukio
- 1932 - Nchi ya Iraq inapata uhuru kutoka Uingereza
- 1990 - Ujerumani umeunganika tena kuwa nchi moja. Mikoa yote ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani inajiunga na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani
Waliozaliwa
- 1458 - Kasimir Mtakatifu, mwana mfalme wa Poland
- 1904 - Charles Pedersen, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1987
- 1947 - Feetham Filipo Banyikwa, mwanasiasa wa Tanzania
Waliofariki
- 1226 - Mtakatifu Fransisko wa Asizi, shemasi, mwanzilishi wa Ndugu Wadogo
- 1929 - Gustav Stresemann, mwanasiasa Mjerumani na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 1926
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Denisi Mwareopago, Kandida wa Roma, Fausto, Kayo na wenzao, Hesiki wa Gaza, Masimiani wa Bagai, Sipriani wa Toulon, Ewadi na Ewadi, Jeradi wa Brogne, Emilia wa Villeneuve n.k.