LIMSwiki
Yaliyomo
Tarehe 27 Julai ni siku ya 208 ya mwaka (ya 209 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 157.
Matukio
Waliozaliwa
- 1835 - Giosue Carducci, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1906
- 1881 - Hans Fischer, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1930
- 1963 - Donnie Yen, mwigizaji wa filamu kutoka Uchina
- 1967 - Rahul Bose, mwigizaji wa filamu kutoka Uhindi
- 1983 - Blandina Changula, mwigizaji filamu kutoka Tanzania
- 1984 - Neema Decoras, mwimbaji kutoka Tanzania
- 1989 - Savio Nsereko, mchezaji mpira kutoka Ujerumani
Waliofariki
- 432 - Mtakatifu Papa Celestino I
- 1061 - Papa Nikolasi II
- 1917 - Emil Theodor Kocher, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1909
- 1948 - Susan Glaspell, mwandishi wa kike kutoka Marekani
- 2008 - Chacha Zakayo Wangwe, mwanasiasa wa Tanzania
- 2016 - James Alan McPherson, mwandishi kutoka Marekani
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Wafiadini saba wa Efeso, Pantaleo wa Nikomedia, Desiree wa Besancon, Papa Selestini I, Simeoni wa Mnarani, Orso wa Loches, Eklesio, Galatori, Antusa wa Eskihisar, Joji, Aureli na wenzao, Klementi wa Ohrid n.k.