LIMSwiki
Yaliyomo
Tarehe 23 Novemba ni siku ya 327 ya mwaka (ya 328 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 38.
Matukio
- 1700 - Uchaguzi wa Papa Klementi XI
Waliozaliwa
- 1804 - Franklin Pierce, Rais wa Marekani (1853-1857)
- 1837 - Johannes Diderik van der Waals, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1910
- 1860 - Karl Hjalmar Branting, mwanasiasa Mswidi na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 1921
- 1922 - Joan Fuster, mwandishi wa Kikatalunya kutoka Hispania
- 1941 - Franco Nero, mwigizaji wa filamu kutoka Italia
- 1971 - Chris Hardwick, mwigizaji wa filamu kutoka Marekani
Waliofariki
- 1814 - Elbridge Gerry, Kaimu Rais wa Marekani
- 1991 - Klaus Kinski, mwigizaji filamu kutoka Ujerumani
- 1996 - Mohamed Amin, mpiga picha kutoka Kenya
- 2012 - Larry Hagman, mwigizaji filamu kutoka Marekani
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Papa Klementi I, Kolumbano, Felisita wa Roma, Mustiola, Sisini wa Kuziko, Klementi wa Metz, Lukresia wa Merida, Anfiloki wa Ikonio, Severini wa Paris, Gregori wa Agrigento, Trudo, Sesilia Yu So-sa n.k.