LIMSwiki
Yaliyomo
Tarehe 21 Septemba ni siku ya 264 ya mwaka (ya 265 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 101.
Matukio
- 1676 - Uchaguzi wa Papa Innocent XI
- 1979 - Serikali ya Jean Bedel Bokassa, Kaisari wa Afrika ya Kati, inapinduliwa
- 1981 - Nchi ya Belize inapata uhuru kutoka Uingereza
- 1991 - Nchi ya Armenia inapata uhuru wake rasmi kutoka Umoja wa Kisovyeti
Waliozaliwa
- 1415 - Kaisari Federiki III wa Ujerumani (1440-1493)
- 1853 - Heike Kamerlingh Onnes, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1913
- 1866 - Charles Nicolle, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1928
- 1909 - Kwame Nkrumah, Rais wa kwanza wa Ghana
- 1926 - Donald A. Glaser, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1960
- 1934 - David James Thouless, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 2016
- 1945 - Kay Ryan, mshairi kutoka Marekani
- 1983 - Anna Favella, mwigizaji wa filamu kutoka Italia
Waliofariki
- 687 - Papa Konon
- 1558 - Kaisari Karoli V wa Ujerumani (1519-1556)
- 1860 - Arthur Schopenhauer, mwanafalsafa wa Ujerumani
- 1971 - Bernardo Houssay, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1947
- 1973 - William Plomer, mwandishi wa Afrika Kusini
- 1987 - Jaco Pastorius, mwanamuziki kutoka Marekani
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha sikukuu ya Mtume Mathayo, na kumbukumbu za watakatifu nabii Yona, Kwadrato wa Athens, Pamfili wa Roma, Aleksanda wa Roma, Eusebi, Nestabo na wenzao, Kastori wa Apt, Kadoko, Landelini wa Ettenheim, Gerulfi, Maura wa Troyes, Fransisko Jaccard, Thomas Tran Van Thien, Laurenti Imbert, Petro Maubant, Yakobo Chastan n.k.