LIMSwiki
Yaliyomo
Mandhari
Tarehe 21 Aprili ni siku ya 111 ya mwaka (ya 112 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 254.
Matukio
- 753 KK - Mji wa Roma kuundwa na Romulo (tarehe ya kimapokeo). Romulo anakuwa mfalme wa kwanza wa Roma hadi 715 KK. Ndio mwanzo wa hesabu ya miaka katika kalenda ya Kiroma: "ab Urbe Condita" = AUC (kwa Kilatini: tangu kuundwa kwa mji)
Waliozaliwa
- 1795 - Mtakatifu Vinsenti Pallotti, padre Mkatoliki kutoka Italia
- 1837 - Fredrik Bajer, mwanasiasa Mdenmark, na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 1908
- 1882 - Percy Bridgman, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1946
- 1889 - Paul Karrer, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1937
- 1926 - Elizabeth II, Malkia wa Uingereza
Waliofariki
- 1073 - Papa Alexander II
- 1109 - Mtakatifu Anselm wa Canterbury, askofu mkuu wa Canterbury (Uingereza), mmonaki na mwalimu wa Kanisa kutoka Aosta (Italia)
- 1894 - Mtakatifu Konrad wa Parzham, bradha Mfransisko nchini Ujerumani
- 1910 - Mark Twain, mwandishi kutoka Marekani
- 1965 - Edward Appleton, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1947
- 1989 - James Kirkwood, mwandishi Mmarekani, na mshindi wa Tuzo ya Pulitzer, mwaka wa 1976
- 2009 - Santha Rama Rau, mwandishi kutoka Uhindi
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Anselm wa Canterbury, Apoloni wa Roma, Aristo, Anastasi wa Sinai, Mael Ruba, Konrad wa Parzham, Romano Adame n.k.
Viungo vya nje
- BBC: On This Day
- On This Day in Canada Archived 2012-12-11 at Archive.today