LIMSpec Wiki
![](https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/16/Louis-Nicolas_Clerambault.jpg/220px-Louis-Nicolas_Clerambault.jpg)
Mtunzi (kutoka kitenzi "kutunga"; kwa Kiingereza: composer, kutoka Kilatini compōnō, yaani "naweka pamoja") ni hasa mwanamuziki ambaye amebuni wimbo au muziki wa aina yoyote. Mara nyingi mtunzi ni pia mwimbaji au mpiga ala bora.
Katika Kiswahili jina hilohilo linaweza pia kutumika kwa mtu aliyeandika kitabu au shairi, lakini pia msanii wa aina nyingine aliyebuni kitu kipya.