LIMSpec Wiki
Yaliyomo
Lango la Historia | Lango la Biografia | Karibuni | Orodha ya Miaka
◄ |
Milenia ya 2 KK |
Milenia ya 1 KK |
Milenia ya 1 |
►
◄ |
Karne ya 3 KK |
Karne ya 2 KK |
Karne ya 1 KK |
Karne ya 1 |
Karne ya 2 |
►
Miaka ya 90 KK |
Miaka ya 80 KK |
Miaka ya 70 KK |
Miaka ya 60 KK |
Miaka ya 50 KK |
Miaka ya 40 KK |
Miaka ya 30 KK |
Miaka ya 20 KK |
Miaka ya 10 KK |
Miaka ya 0 KK
Karne ya 1 KK huhesabiwa kuanzia tarehe 1 Januari 100 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 1 KK.
Matukio
Karne hii iliona matukio yaliyoendelea kuwa muhimu katika kipindi kilichofuata.
- Dola la Roma lilipata kipaumbele katika Ulaya na eneo la Mediteranea kwa karne zilizofuata, likifuata mtindo wa utawala wa Kaisari badala ya jamhuri
- Misri ilikwisha kama nchi ya kujitawala ikaendelea kuwa jimbo la madola makubwa yaliyofuatana kwa karne 19.
- Mamlaka ya Nasaba ya Han katika China yaanza kuporomoka
- Yesu alizaliwa na Bikira Maria takriban 7-5 KK huko Bethlehemu (Palestina)
Watu muhimu
- Cicero, mwanafalsafa, mwanasiasa na mwandishi wa Kilatini
- Julius Kaisari (100 KK-44 KK), mtawala wa Roma hadi alipouawa
- Kaisari Augusto (63 KK-14), mtawala wa Roma aliyerudisha amani ya kudumu
- Herode Mkuu, mfalme wa Israeli chini ya himaya ya Dola la Roma (37 KK-4 KK)
- Maria wa Nazareti, mama wa Yesu