LIMSpec Wiki
Yaliyomo
Mandhari
Tarehe 6 Julai ni siku ya 187 ya mwaka (ya 186 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 178.
Matukio
- 1758 - Uchaguzi wa Papa Klementi XIII
- 1964 - Nchi ya Malawi inapata uhuru kutoka Uingereza
- 1975 - Visiwa vya Komori vinapata uhuru kutoka Ufaransa
Waliozaliwa
- 1859 - Verner von Heidenstam, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1916
- 1903 - Hugo Theorell, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1955
- 1907 - Frida Kahlo, mchoraji kutoka Mexiko
- 1937 – Bessie Head, mwandishi wa Afrika Kusini na Botswana
- 1946 - George W. Bush, Rais wa Marekani (2001-2009)
- 1970 - Inspectah Deck, mwanamuziki kutoka Marekani
- 1982 - Tay Zonday, mwigizaji wa filamu kutoka Marekani
Waliofariki
- 1535 - Mtakatifu Thomas More, mwanasheria kutoka Uingereza, aliuawa kwa imani yake
- 1902 - Mtakatifu Maria Goretti, bikira mfiadini wa Italia
- 1962 - William Faulkner, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1949
- 1971 - Louis Armstrong, mpuliza tarumbeta wa Jazz
- 2005 - Claude Simon, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1985
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Maria Goretti, Siriaka wa Nikomedia, Romolo wa Fiesole, Sisoi Mkuu, Paladi wa Uskoti, Moninne, Goar, Yusto wa Condat, Petro Wang Zuolong, Nazaria Ignasya n.k.