LIMSpec Wiki
Yaliyomo
Mandhari
Tarehe 13 Mei ni siku ya 133 ya mwaka (ya 134 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 232.
Matukio
- 1572 - Uchaguzi wa Papa Gregori XIII
- 1607 - Wafanyabiashara Waingereza waunda mji wa Jamestown, Virginia utakaokuwa kituo cha kwanza cha kudumu cha Uingereza katika Amerika ya Kaskazini na chanzo cha Marekani.
Waliozaliwa
- 1655 - Papa Innocent XIII
- 1792 - Mwenye heri Papa Pius IX, aliyeongoza Kanisa Katoliki muda mrefu kuliko wote
- 1857 - Sir Ronald Ross, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1902
- 1950 - Stevie Wonder, mwanamuziki wa Marekani
- 1972 - Giovanni Tedesco, mchezaji mpira wa Italia
Waliofariki
- 1930 - Fridtjof Nansen, mpelelezi na mwanasiasa Mnorwei, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 1922
- 2001 - Jason Miller, mwandishi na mwigizaji filamu kutoka Marekani
- 2006 - Peter Viereck, mshairi kutoka Marekani
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Bikira Maria wa Fatima, Servasi, Agnes wa Poitiers, Andrea Hubati Fournet n.k.