LabLynx Wiki
Yaliyomo
Jinsia | mume |
---|---|
Nchi ya uraia | Brazil, Hispania, Uingereza |
Nchi anayoitumikia | Brazil |
Jina katika lugha mama | Casemiro |
Jina la kuzaliwa | Carlos Henrique Casimiro |
Jina halisi | Carlos Henrique |
Jina la familia | Casimiro |
Tarehe ya kuzaliwa | 23 Februari 1992 |
Mahali alipozaliwa | São José dos Campos |
Lugha ya asili | Kireno |
Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihi | Kireno |
Kazi | association football player |
Nafasi anayocheza kwenye timu | Kiungo |
Makazi | São José dos Campos |
Muda wa kazi | 25 Julai 2010 |
Mchezo | mpira wa miguu |
Namba ya Mchezaji | 14 |
Ameshiriki | Kombe la Dunia la FIFA 2018, 2019 Copa América |
Carlos Henrique Casimiro (anajulikana kama Casemiro; alizaliwa 23 Februari 1992) ni mchezaji wa soka wa Brazil ambaye anacheza kama kiungo mkabaji katika klabu ya Hispania ya Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil.
Ametokea huko São Paulo, ambapo alifunga mabao 11 katika michezo 112 rasmi, alihamia Real Madrid mwaka 2013, na pia alitumia msimu alikokwenda kwa mkopo huko Porto. Alikuwa kwenye kikosi cha Real Madrid kikosi kilichoshinda Ligi ya Mabingwa mara tatu, kutoka 2013-2014 hadi 2016-2018.
Upande wa kitaifa, alianza kuichezea timu ya Brazil toka mwaka 2011,akishiriki michuano ya Copa America miaka ya 2015 na 2016 na pia kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2018.
Ngazi ya klabu
São Paulo
Alizaliwa São José dos Campos, São Paulo, Casemiro alikuwa ni matunda ya akademi ya São Paulo FC.Akiwa na umri wa maka 11 na zaidi alikuwa kama nahodha wa timu.Alijulikana kama "Carlão" ambayo ni moja ya matamshi ya jina lake la kwanza kwa kireno.
Casemiro aliisaidia timu yake ilipoelemewa kwa kufunga goli lake la kwanza na kuisaidia timu yake kusuluhu 2-2 dhidi ya Cruzeiro Esporte Clube. Tarehe 7 Aprili 2012, Casemiro alifunga goli lake la kwanza la ushindi wa 2-1 kwenye uwanja wa Arena Barueri dhidi ya Mogi Mirim Esporte Clube alipocheza nafasi ya Fabrício aliyeumia.
Real Madrid
Januari 2013,Casemiro alipelekwa kwa mkopo kwenda Real Madrid Hispania alipojiunga na timu 'B'.Alicheza mechi yake ya kwanza 16 Februari walipopigwa 3-1 na CE Sabadell FC.
Casemiro alianza mafanikio yake Real Madrid alipocheza dakika 90 ambapo walishinda 3-1 dhidi ya Real Betis.Juni 2 alishinda goli lake la kwa nza akiwa Ulaya,siku nane baadaye alinunuliwa jumla kwa mkataba wa miaka minne R$18.738 milioni.