LabLynx Wiki
Yaliyomo
Mandhari
Tarehe 9 Desemba ni siku ya 343 ya mwaka (ya 344 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 22.
Matukio
- 1961 - Nchi ya Tanganyika inapata uhuru kutoka Uingereza, huku ikiendelea kuwa na Elizabeti II kama malkia wake kwa mwaka mmoja
Waliozaliwa
- 1868 - Fritz Haber, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1918
- 1917 - James Rainwater, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1975
- 1919 - William Lipscomb, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1976
- 1919 - Mary Benson, mwandishi wa kike wa Afrika Kusini
- 1926 - Henry Kendall, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1990
- 1952 - Ludovic Minde, askofu Mkatoliki nchini Tanzania
- 1957 - Jacob Venance Koda, askofu Mkatoliki nchini Tanzania
Waliofariki
- 1437 - Kaisari Sigismund wa Ujerumani
- 1565 - Papa Pius IV
- 1669 - Papa Klementi IX
- 1937 - Nils Dalen, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1912
- 1945 - Yun Chi-ho, mwanasiasa kutoka Korea Kusini
- 1971 - Ralph Bunche, mwanasiasa Mmarekani, na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 1950
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Juan Diego, Leokadia wa Toledo, Siro wa Pavia, Gorgonia wa Nazienzi, Sipriani wa Genouillac, Petro Fourier n.k.