LabLynx Wiki
Yaliyomo
Tarehe 29 Julai ni siku ya 210 ya mwaka (ya 211 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 155.
Matukio
Waliozaliwa
- 1869 - Booth Tarkington, mwandishi kutoka Marekani
- 1898 - Isidor Rabi, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia, mwaka wa 1944
- 1900 - Eyvind Johnson, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1974
- 1905 - Stanley Kunitz, mshairi kutoka Marekani
- 1918 - Edwin O'Connor, mwandishi kutoka Marekani
- 1938 - Enzo G. Castellari, mwongozaji wa filamu kutoka Italia
- 1981 - Fernando Alonso, dereva wa Formula One kutoka Hispania
Waliofariki
- 238 - Balbinus, Kaisari wa Dola la Roma aliuawa
- 238 - Pupienus, Kaisari wa Dola la Roma aliuawa
- 1099 - Mwenye heri Papa Urban II
- 1644 - Papa Urban VIII
- 1856 - Robert Schumann, mtunzi wa muziki kutoka Ujerumani
- 1890 - Vincent van Gogh, mchoraji kutoka Uholanzi
- 1913 - Tobias Asser, mwanasheria Mholanzi, na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 1911
- 1994 - Dorothy Hodgkin, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1964
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu ya watakatifu Martha, Maria na Lazaro wa Bethania, Kaliniko wa Gangra, Felisi wa Roma, Simplisi, Faustini na wenzao, Lupo wa Troyes, Prospa wa Orleans, Olaf II, Wiliamu Pinchon, Yosefu Zhang Wenlan, Paulo Chen Changpin, Yohane Mbatizaji Luo Tingyin, Martha Wang Luoshi n.k.