Clinfowiki

Mwendo wa injini ya mwako ndani ya mapigo manne. Pigo 1: pistoni inarudi nyuma na kuongeza nafasi katika silinda, hewa na fueli zinavutwa ndani ya silinda, pigo 2: pistoni inasogea mbele na kupunguza nafasi ndani ya silinda, mchanganyiko wa hewa na fueli hukandamizwa, pigo 3: mchanganyiko hulipuka, silinda inasukumwa na nguvu ya mlipuko na kuzungusha mtaimbo endeshi, pigo 4: pistoni inasogea mbele na kusukuma gesi zilizochomwa nje

Injini ya mwako ndani ni aina ya injini ambako fueli huchomwa ndani yake. Kuchomwa wa fueli kama vile petroli, diseli au gesi katika mchanganyiko na hewa huachisha nishati yake kwa umbo la joto na shinikizo. Gesi ya mwako pamoja na hewa hupanuka kwa njia hii na kusukuma sehemu za injini hasa pistoni zinazopeleka nguvu ya mwako hadi mtaimbo endeshi ya injini. Kutoka hapa nguvu ya mwendo unapelekwa mahali panapohitajika.

Kuna injini zenye mfumo tofauti zisizohesabiwa kati ya injini za mwako ndano kwa mfano injini ya mvuke. Hapo fuelli huchomwa na mvuke kutengenezwa nje ya injini yenyewe kwa hiyo ni injini ya mwako nje.

Muundo wa injini ya mwako ndani

Kila injini ya mwako ndani inafuata hatua mbalimbali zinazorudiarudia. Kuna hasa mfumo wa mapigo mawili na mapigo manne, na injini nyingi ya magari ni ya mapigo manne.

Kila injini huwa na silinda ambayo ni chumba cha kuchoma fueli. Kuna injini za silinda 1, mara nyingi 4 au pia zaidi. Kuchoma kwa fueli kunazalisha gesi inayopanuka na kuleta shinikizo kubwa. Ndani ya silinda kuna pistoni inayosukumwa kwa nguvu ya gesi inayaotokea kutokana na kuchomwa kwa fueli. Mwendo wa pistoni inapelekwa kwa mtaimbo wa injini.

Injini ya mwako ndani inahitaji nafasi ya kuingiza fueli na hewa pamoja na uwezo wa kutoa gesi iliyozalishwa wakati wa mwako wa fueli.

Fueli inaingizwa katika silinda kwa umbo la matone madogo na hii inafanywa kwa kuipitisha katika nozeli yaani shimo ndogo sana. Pampu ya injekta inapima kiwango cha petroli kinachotakiwa. Matone madogo ya fueli yanachanganywa na hewa na mchaganyiko huu unawaka. Kwa njia nyingine kuna pia injini ambako fueli na hewa zinachanganywa nje ya injini katika kabureta na mchanganyiko ulio tayari navutwa ndani ya silinda inapowaka.

Kuna namna mbili za kuwasha mchanganyiko wa hewa na fueli mara nyingi kuna plagi inayotoa cheche ya moto wakati mchanganyiko wa fueli na hewa imeshakandamizwa. Njia nyingine inayotumiwa katika injini za diseli ni kuongeza shinikizo ndani ya silinda na kukandamiza hewa ndai ya silinda sana hadi hewa hii imekuwa joto sana na sasa matone ya diseli zinapulizwa na kuwaka kutokana na joto la hewa.

Wakati wa kuwaka fueli pamoja na oksijeni ya hewa zinaunda gesi inayopanuka haraka. Nguvu hii inasukuma dhidi ya pistoni inayorudishwa nyuma; ilhali imeunganishwa na mtaimbo wa injini inasukuma mtaimbo na hivyo kuzungusha injini yote.

Mwendo wa injini inaendelea kusukuma pistoni tena katika hali ya awali ambako inapuliza gesi za mwako nje kupitia valvu ya kutoka.

Injini ya mwako ndani inazungushwa na pistoni zake na idadi ya mizunguko inafikia mara 1000 hadi 8000 kila dakika. Maana kila pistoni inasogea mbele na nyuma mara alfu nyingi ila dakika. Hapo ni muhimu ya kwamba msuguano kati ya sehemu zake inapunguzwa kiasi jinsi kinavyowezekana na kazi hii inatekelezwa na mafuta ya injini inayosaidia kutelezesha vipande vyote vyenye mwendo. Kila injini ya mwako ndani huwa na nafasi kwa ajili ya mafuta ya kutelezesha vipande vyake.

Vilevile ni muhimu ya kwamba vipande vyote vinaingiana vema na visiwe na nafasi kubwa ya kucheza. Hapo ni muhimu ya kwmaba vipimo vya vipuri vyote vinafaa na kulingana hadi sehemu ya 100 ya milimita.

Mfumo wa kupoza

Vilevile ni muhimu ya kwamba joto la injini linapunguzwa. Maana ndani ya injini moto unawaka muda wote na kuathiri metali ya injini yenyewe. Hapo injini inahitaji na mfumo wa kupoza.

Mara nyingi kazi hii inatekelezwa kwa kuzungusha miminiko kama maji katika injini inayopita sehemu penye joto kubwa; maji hupokea sehemu ya joto na kuibeba nje ya injini yenyewe hadi sehemu ya rejeta yanapopozwa kwa kukutana na hewa kutoka nje ya gari.

Injini ndogo, siku hizi hasa za pikipiki, hutumia kupoza kwa hewa; uso wa injini huongezwa kwa mapezi ya kupoza ambako hewa inapita moja kwa moja ikitawanya joto.