Clinfowiki
Yaliyomo
Mandhari
Tarehe 31 Oktoba ni siku ya 304 ya mwaka (ya 305 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 61.
Matukio
- 1517 - Martin Luther anatolea "Hoja 95 dhidi ya madekezo": ndio mwanzo wa Matengenezo ya Kiprotestanti
- 1919 - Nchi ya Iraq inapata uhuru kutoka Uturuki
Waliozaliwa
- 1618 - Mtakatifu Maria Ana wa Yesu, bikira Mfransisko kutoka Ekwador
- 1705 - Papa Klementi XIV
- 1835 - Adolf von Baeyer, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1905
- 1880 - Julia Peterkin, mwandishi kutoka Marekani
- 1920 - Dedan Kimathi, kiongozi wa Mau Mau nchini Kenya
- 1925 - John Pople, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1998
- 1929 - Bud Spencer, mwigizaji wa filamu kutoka Italia
- 1973 - Beverly Lynne
- 1990 - JID, rapa wa Marekani
Waliofariki
- 1960 - Harold L. Davis, mwandishi kutoka Marekani
- 1986 - Robert Mulliken, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1966
- 1993 - Federico Fellini, mwongozaji wa filamu kutoka Italia
- 2006 - Pieter Willem Botha, Waziri Mkuu na Rais wa Afrika Kusini
- 2020 - Sean Connery
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Epimako wa Pelusi, Kwintino, Foilano, Antonino wa Milano, Volfang wa Regensburg, Alfonso Rodriguez n.k.
Viungo vya nje
- BBC: On This Day Archived 12 Machi 2007 at the Wayback Machine.