Bioinformatics Wiki
Yaliyomo
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: God Defend New Zealand (Mungu Ilinde New Zealand) God Save the King | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Wellington | ||||
Mji mkubwa nchini | Auckland | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza (95.9%) Kimaori (4.2%) | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba Charles III wa Uingereza Cindy Kiro Chris Hipkins | ||||
Uhuru Dominion (kujitawala) |
26 Septemba 1907 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
268,680 km² (ya 75) 2.1 | ||||
Idadi ya watu - October 2021 kadirio - 2018 sensa - Msongamano wa watu |
5,132,870 (ya 123) 4,699,755 19.1/km² (ya 167) | ||||
Fedha | New Zealand dollar (NZD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
NZST9 (UTC+12) NZDT (UTC+13) | ||||
Intaneti TLD | .nz10 | ||||
Kodi ya simu | +64
- |
Nyuzilandi (kwa Kiingereza: New Zealand; kwa Kimaori: Aotearoa) ni nchi ya visiwani katika Pasifiki takriban km 1,500 upande wa mashariki-kusini wa Australia.
Eneo lake linaundwa na visiwa viwili vikubwa: Kisiwa cha Kaskazini (North Island au Te Ika-a-Māui) na Kisiwa cha Kusini (South Island au Te Waipounamu) na vingine 600 vidogo.
Jiografia
Miji
- Wellington ni mji mkuu wa Nyuzilandi.
- Auckland ndio mji mkubwa visiwani.
Miji mingine ni:
- Christchurch
- Hamilton
- Dunedin
- Tauranga
- Lower Hutt
- Palmerston North
- Napier
- Nelson
- Rotorua
- Invercargill
- New Plymouth
- Porirua
- Upper Hutt
- Whanganui
- Gisborne
Watu
Idadi ya wakazi ni 4,690,000. Wengi wao (74%) bado wana asili ya Ulaya, ingawa asilimia yao inazidi kupungua. Wakazi asilia ni Wamaori waliotokea Polinesia na kuhamia visiwa hivyo kati ya miaka 1250-1300 BK; kwa sasa ni 14.9% ya wakazi wote. Wengine wana asili ya Asia (11.8%) na ya visiwa vya Pasifiki (7.4%).
Lugha rasmi ni Kiingereza, Kimaori na Lugha ya Ishara ya Nyuzilandi (kwa Kiingereza: New Zealand Sign Language au NZSL).
Upande wa dini, 49% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Kanisa Katoliki (12.6%), Anglikana (11.8%) na Wapresbiteri (8.5%). Idadi ya wasio na dini inazidi kupanda na imeshafikia 38.55%, mbali ya 12.27% wasiojibu swali kuhusu hilo. Kuna Mabanyani (2.1%), Wabuddha (1.5%), Waislamu (1.2%), Singasinga (0.5%)
Tazama pia
Viungo vya nje
- (Kiingereza) Tovuti rasmi Archived 13 Agosti 2007 at the Wayback Machine.
Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki |
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polinesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna |