Bioinformatics Wiki
Yaliyomo
Barua kwa Waefeso ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya ambalo pamoja na Agano la Kale linaunda Biblia ya Kikristo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Mazingira
Mtume Paulo aliweza kuandika barua hii akiwa kifungoni Roma kati ya miaka 61 na 63 ili isomwe katika makanisa yote ya mkoa wa Asia Ndogo, wenye makao makuu mjini Efeso.
Mada
Mafundisho yake yanalingana na yale ya barua kwa Wakolosai ila yamechimbwa zaidi, kiasi kwamba barua hii inaonekana kuwa kilele cha teolojia ya Paulo.
Pamoja na kuchambua fumbo la wokovu katika Yesu Kristo, inachambua hasa fumbo la Kanisa kama mwili wa Kristo ambamo kichwa kinaeneza wokovu ulimwenguni kote.
Kwa msingi huo inasisitiza na kudai umoja kamili kati ya waamini (Ef 1:1-2; 1:17-23; 2:11-22; 3:1-21; 4:1-16).
== Viungo vya nje ==
Wikisource has original text related to this article: |
Tafsiri ya Kiswahili
- [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili
Vingine
- A Brief Introduction to Ephesians Archived 6 Septemba 2015 at the Wayback Machine.
- Ephesians Online Reading Room Archived 13 Mei 2017 at the Wayback Machine. – extensive collection of online resources for Ephesians; Tyndale Seminary
- Biblical Expository on Ephesians Archived 4 Februari 2017 at the Wayback Machine.
- Ephesians: The Calling of the Saints – Ephesians Messages, Audio & Podcast by Ray Stedman