Trends in LIMS
Yaliyomo
Tarehe 2 Novemba ni siku ya 306 ya mwaka (ya 307 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 59.
Matukio
- 1389 - Uchaguzi wa Papa Boniface IX
Waliozaliwa
- 1795 - James Polk, Rais wa Marekani (1845-1849)
- 1865 - Warren G. Harding, Rais wa Marekani (1921-1923)
- 1883 - Martin Flavin, mwandishi kutoka Marekani
- 1911 - Odysseas Elytis, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1979
- 1929 - Richard Taylor, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1990
- 1932 - Melvin Schwartz, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1988
- 1946 - Marieta Severo, mwigizaji wa filamu kutoka Brazil
- 1978 - Noah Ngeny, mwanariadha kutoka Kenya
Waliofariki
- 1950 - George Bernard Shaw, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1925
- 1966 - Peter Debye, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1936
- 1994 - Peter Taylor, mwandishi kutoka Marekani
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za Marehemu wote, lakini pia za watakatifu Vitorini wa Ptuj, Yusto wa Trieste, Karteri na wenzake, Asidini na wenzake, Donini wa Vienne, Marsiano wa Kalsedonia, Ambrosi wa Agaune, Winifrida, Joji wa Vienne, Malakia wa Armagh n.k.