Trends in LIMS
Yaliyomo
Mandhari
Tarehe 17 Agosti ni siku ya 229 ya mwaka (ya 230 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 136.
Matukio
- 1740 - Uchaguzi wa Papa Benedikto XIV
- 1945 - Nchi ya Indonesia inatangaza uhuru wake kutoka Uholanzi
- 1960 - Nchi ya Gabon inapata uhuru kutoka Ufaransa
Waliozaliwa
- 1844 - Menelik II, mfalme mkuu wa Uhabeshi
- 1932 - Vidiadhar Naipaul, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi, mwaka wa 2001
- 1871 - Jesse Lynch Williams, mwandishi kutoka Marekani
- 1932 - Abebe Bikila, mwanariadha Mhabeshi
- 1941 - Ibrahim Babangida, Rais wa Nigeria (1985-1993)
- 1945 - Norbert Wendelin Mtega, askofu Mkatoliki nchini Tanzania
Waliofariki
- 1304 - Go-Fukakusa, mfalme mkuu wa Japani (1246-1259)
- 1633 - Mtakatifu Yakobo Kyushei Tomonaga, O.P., padri na mfiadini kutoka Japani
- 1969 - Otto Stern, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1943
- 1982 - Ruth First, mwandishi wa Afrika Kusini
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Miro wa Kuziko, Mamas wa Kaisarea, Papa Eusebius, Jero, Elia Kijana, Nikola Politi, Klara wa Montefalco, Beatriz wa Silva, Yakobo Kyushei Tomonaga, Mikaeli Kurobioye, Yoana Delanoue n.k.
Viungo vya nje
- BBC: On This Day
- On This Day in Canada Archived 2012-12-09 at Archive.today