Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.
Chuo ni taasisi ya elimu ya pekee. Inatoa mafunzo ya kazi fulani. Mifano ni chuo cha ufundi, chuo cha kilimo au chuo cha ualimu. Kwa kila namna chuo kinaanza kufundisha watu baada ya kumaliza ngazi fulani ya shule.
Kiasili maana ya neno "chuo" ilikuwa sawa na "kitabu". Kwa maana hiyo linatumiwa kwa mfano katika tafsiri za Biblia kama vile Injili ya Luka 4:17 "Yesu akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo".[1]
Kutokana na maana hii asilia "chuo" kimekuwa pia neno la kutaja mahali pa kujifunza kusoma, kwa hiyo katika Kiswahili cha miaka iliyopita kiliweza kutaja pia shule.[2].
Leo hii matumizi ya neno yamebadilika, kwa maana ya "kitabu" hupatikana tu katika matini zenye Kiswahili cha zamani na kama mahali au taasisi ya elimu kwa jumla, neno "shule, skuli"[3] limechukua nafasi pana zaidi.
Jina la "Chuo" linaweza kutaja taasisi zinazotoa elimu kwa ngazi tofauti sana. Hii itategemea na muundo wa elimu katika nchi mbalimbali.
Watu wanaoingia katika chuo kwa shabaha ya kujifunza huitwa wanafunzi, pia wanachuo au wanazuo(ni). Wale wanaotoa elimu huitwa walimu, kwenye ngazi za juu zaidi wanaweza kuitwa pia profesa au wakufunzi.
Nchini Tanzania vyuo huratibiwa na tume ya vyuo vikuu nchini humo inayoitwa TCU (Tanzania commission for university).[5] Tume ya vyuo vikuu Tanzania imeonyesha orodha ya vyuo nchini Tanzania kwamba mpaka mnamo waka 2019 Tanzania ilikua tayari na vyuo zaidi ya hamsini (50), Orodha ya vyuo vilivo idhinishwa ta tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania (bofya hapa) Archived 5 Desemba 2020 at the Wayback Machine..