Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.
Kundinyota | Kinubi (Lyra) |
Mwangaza unaonekana | +0.026 |
Kundi la spektra | A0 Va |
Paralaksi (mas) | 130.23 ± 0.36 |
Umbali (miakanuru) | 25 |
Mwangaza halisi | +0.582 |
Masi M☉ | 2.13 |
Nusukipenyo R☉ | 2.3 |
Mng’aro L☉ | 40.12 |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | 9600 |
Muda wa mzunguko | masaa 12.5 |
Majina mbadala | Wega, Lucida Lyrae, Alpha Lyrae, α Lyrae, 3 Lyr, BD+38°3238, GCTP 4293.00, HD 172167, GJ 721, HIP 91262, HR 7001, LTT 15486, SAO 67174 |
Vega au α Alfa Lyrae ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Shaliaki (kwa Kiingereza Lyra) na kati ya nyota angavu sana kwenye anga ya usiku.
Jina linatokana na Kiarabu النسر الواقع al-nasr al-waqi, hasa kutoka sehemu ya pili واقع ambamo herufi ya ق q ilichukuliwa kama "g" na hivyo kuleta "Vega" kwa tahajia ya Kilatini. Hili ni jina lililokubaliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia[1].
Vega ni nyota ya safu kuu inayoyeyunganisha hidrojeni kuwa heliamu ndani ya kiini chake. Masi yake ni zaidi ya mara mbili ya masi ya Jua. Ilhali nyota kubwa huchoma fueli yake ya myeyungano haraka kuliko nyota ndogo zaidi Vega itakuwa na maisha mafupi kuliko Jua. Kwa sasa mwangaza halisi ni mara kumi ya Jua. Inazunguka haraka kwenye mhimili wake.
Hadi sasa sayari zinazozunguka Vega hazikuthibitishwa. Lakini kuna dalili ya kwamba kuna mata inayozunguka nyota iliyo katika mchakato ya kujikaza kuwa sayari [2]
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vega kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa . |