Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.
Ufinyanzi ni teknolojia na ufundi wa kutengeneza vyombo kwa matumizi ya binadamu kwa kutumia udongo wa mfinyanzi au kauri.
Udongo wa ufinyanzi unapewa umbo unaotakiwa, kukaushwa, kupambwa na kuchomwa kwa moto na kwa njia hii vyombo vigumu vinatokea kwa matumizi yanayotakiwa kama vile sahani, bakuli, chungu, kikombe au birika.
Udongo wa aina ya ufinyanzi ni udongo wa pekee ambao una chembechembe ndogo sana. Chembe zake ni ndogo kuliko mikromita 2. Unapokea maji na kuyashika ndani yake na katika hali ya unyevu ni laini sana una tabia ya kushikamana. Tabia hii inamruhusu mfinyanzi kuupa maumbo mbalimbali.
Lakini baada ya kukauka unakuwa mgumu. Ukichomwa motoni ugumu unaongezeka pia uwezo wake wa kuvumilia kanieneo.
Kuna mbinu mbalimbali za kufinyanga vyombo.