Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.
Reggae (tamka: "rege") ni aina ya muziki kutoka nchini Jamaika. Ilianzishwa mwaka 1968 na kuwa maarufu kimataifa kwa nyimbo za Bob Marley na kundi lake The Wailers. Pia watu kama Lucky Dube na John Tosh waliwezesha reggae kuwa maarufu.
Reggae hupendwa sana na watu wenye imani ya Rastafari lakini pia watu wa rika, imani na mataifa mbalimbali kote duniani.
Vifaa vya kawaida katika bendi ya Reggae ni ngoma, gitaa ya besi, gitaa na kibodi pamoja na sauti za waimbaji.