Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.
Plutoni (plutonium) | |
---|---|
kipande duara cha plutoni
| |
Jina la Elementi | Plutoni (plutonium) |
Alama | Pu |
Namba atomia | 94 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 244 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 24, 8, 2 |
Densiti | 19.816 g·cm³ |
Kiwango cha kuyeyuka | 912.5 K (639.4 °C) 912,5 K ( °C) |
Kiwango cha kuchemka | 3505 K (3228 °C) K (3228 °C, |
Asilimia za ganda la dunia | 2 · 10-16 % |
Hali maada | mango |
Mengineyo | nururifu sana |
Plutoni ni elementi katika mfumo radidia yenye alama Pu. Namba atomia ni 94 na uzani atomia ni 244. Jina limechaguliwa kutokana na sayari kibete Pluto.
Plutoni ni metali nururifu. Kiasili inatokea katika viwango vidogo sana penye madini ya urani kutokana na mbunguo nyuklia wa elementi hiyo ambao unaweza kuzalisha elementi nyingine. Vile viwango vidogo haviwezi kukaa mud mrefu kutokana na nusumaisha fupi ya plutoni inayozalishwa humo. Sehemu kubwa iliyopo leo hii imezalishwa katika matanuri ya nyuklia kutokana na urani.
Matumizi yake ni katika matanuri ya nyuklia na katika silaha za nyuklia. Matumizi yake ya kijeshi yalitangulia matumizi mengine: bomu lililobomoa mji wa Nagasaki nchini Japan katika Agosti 1945 na kusababisha vifo 60,000 lilitengenezwa kwa plutoni.
Inatokea mara kwa mara kwa kuchoma urani katika tanuri nyuklia. Hivyo inasafishwa na kurudishwa kama fueli katika aina tofauti za matanuri ya nyuklia.
Matatizo yake ni kwamba unururifu wake ni mkali na hivyo kuna hatari ya kuishughulikia katika matumizi. Viwango vidogo sana vya plutoni vinaweza kusababisha kansa kama elementi hii inaingia mwilini kama vumbi au katika chakula. Baada ya kuzalishwa Plutoni inaendelea kuwa nururifu kwa muda mrefu na hivyo takataka ya kinyuklia yenye plutoni inahitaji kutunzwa mbali na watu kwa vipindi wa miaka elfu hata makumi elfu kadhaa.
Matumizi ya pekee ya plutoni ni katika beteri kwa ajili ya vyombo vya angani hasa vile vinavyokwenda mbali na jua na hivyo haviwezi kutumia nishati ya jua.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Plutoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa . |
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Plutoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa . |