Search for LIMS content across all our Wiki Knowledge Bases.
Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.
Picha ya skrini (pia: kielelezo-skrini) ni skrinishoti ya kompyuta. Katika Windows ni kazi rahisi kabisa.
Matumizi
Inasaidia
Kushika makosa yanayotokea wakati wa kutumia programu za kompyuta
Kunakili picha ambazo hazipatikani kwa njia nyingine
Mawasiliano na maelewano kati ya watumiaji wa kompyuta wakiwasiliana kwa njia ya barua pepe
Namna ya kufanya picha kwa kutumia kibodi
Chagua ukurasa au mwandishi au yale unayotaka kuonyesha na hakikisha yameonekana kwenye skrini cha kompyuta yako
Halafu fungua programu ya picha - kwa mfano "paint" (ama kupitia Start-All Programs-Accessories-paint AU kupitia start-run - mspaint).
Kwenye dirisha unalotaka kuonyesha bofya "print screen" (kwa kawaida juu upande wa kulia kwenye sehemu ya kibodi kwa tarakilishi zingine huandikwa kwa kifupi "prt sc" na kwa vifaa zisizo na kibodi vidunde za kuongezea na kupunguza sauti hutumika[1]). Hutaona badiliko lakini umenakili tayari picha ya skrini yako katika kumbukumbu ya muda.
Katika paint (au programu nyingine ya picha) tekeleza amri ya "paste" (kwa menu edit-paste AU kwa puku right click-paste AU kwa kushika CTRL halafu bofya V).
Amri hii inaingiza picha ya skrini katika dirisha la paint.
Picha hii awali bado si imara, unaweza kuisukuma. Bofya "Esc" halafu ni imara.
Sasa unakata sehemu ile tu ambayo unaitaka kuonyesha halafu unainakili na kuiweka kwa ukurasa mpya ya paint.
Ukurasa huu unahifadhi kama picha ukichagua format ya jpg.
Ukihariri picha unaweza pia kuchora duara nyekundu mahali unapotaka kuonyesha hasa.
Hii faili ya picha unaweza kutuma kwa barua pepe au kuingiza katika wikipedia.
TAHADHARI: Usisahau kubadilisha format kuwa jpg au kile unachotaka kwa sababu pekee yake inaweza kuwa faili kubwa sana ya format ya bmp.