Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.
Mitume wa Yesu |
---|
|
Bartolomayo (kwa Kigiriki Βαρθολομαιος) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu kadiri ya Injili Ndugu.
Wengi wanaona hilo ni ubini wake (kwa Kiaramu lina maana ya "mwana wa Tolomayo"), kumbe jina lake mwenyewe ni "Natanaeli", kama anavyotajwa na Injili ya Yohane 1:45, rafiki wa Mtume Filipo. Kama ni hivi, alikuwa mwenyeji wa Kana ya Galilaya, na unyofu wake ulisifiwa na Yesu mara alipokutana naye kwenye mto Yordani.
Anaheshimiwa na madhehebu karibu yote ya Ukristo kama mtakatifu, hasa tarehe 24 Agosti[1].
Yote tunayoyajua kwa hakika juu yake yanategemea Injili na Matendo ya Mitume anapotajwa tu katika orodha ya Thenashara ambao waliteuliwa na Yesu Kristo kama mwanzo mpya wa taifa la Mungu wakatumwa naye kuhubiri na kuponya.
Baada ya ufufuko wa Yesu na Pentekoste, hakuna habari za hakika, ila kuna masimulizi ya utume wake Mashariki ya Kati hadi India[2].
Alifia dini ya Ukristo katika nusu ya pili ya karne I labda Syria au Armenia kama si India.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtume Bartolomayo kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa . |