Knowledge Base Wiki

Search for LIMS content across all our Wiki Knowledge Bases.

Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.

Kwa maana tofauti ya jina hili angalia makala ya maana Moshi


Mji wa Moshi
Mji wa Moshi is located in Tanzania
Mji wa Moshi
Mji wa Moshi

Mahali pa mji wa Moshi katika Tanzania

Majiranukta: 3°20′24″S 37°20′24″E / 3.34000°S 37.34000°E / -3.34000; 37.34000
Nchi Tanzania
Mkoa Kilimanjaro
Wilaya Moshi Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 221,733
Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi mjini
Msikiti Mkuu wa Moshi

Moshi ni makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.

Wakazi

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, mji huo una wakazi wapatao 184,292. Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 331,733 [1].

Kabila linaloongoza kwa idadi ya wakazi wa mji wa Moshi ni Wachagga wakifuatiwa na Wapare na makabila mengine yaliyohamia kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania kama Wasambaa, Warangi n.k. Wachagga wanapenda vyakula vinavyopikwa kwa kutumia ndizi kama vile mtori, kitawa, na machalari.

Wakazi wengi wa Moshi ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara. Watu wengi wanakwenda Moshi kufanya kazi na kurudi nyumbani jioni.

Ukuaji wa mji wa Moshi hauendani na mipango halisi ya 'Mipango Miji'. Hii inatokana na kutokufuatiliwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu uendelezaji wa miji.

Hali ya hewa

Moshi ni mji wenye baridi katika miezi ya Juni mpaka Agosti na joto katika miezi ya Oktoba hadi katikati ya Januari.

Utalii

Mji wa Moshi una mandhari nzuri ya kuvutia watalii. Watalii hupenda sana mji wa Moshi kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na huduma muhimu kama mahoteli na usafiri.

Kampuni nyingi za utalii zimekuwa zikiendesha shughuli zake miaka na miaka. Shughuli kuu za utalii zikiwa ni kupanda mlima Kilimanjaro na kwenda mbuga za wanyama kama vile Serengeti, Ngorongoro, Tarangire na Ziwa Manyara.

Elimu

Mji wa Moshi una vyuo vikuu vinne:

  • MUCCoBS (Moshi University College Of Cooperative and Business Studies) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha Sokoine University of Agriculture (SUA) ya Morogoro
  • MWUCE (Mwenge University College Of Education) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha SAUT (St. Augustine University - Mwanza)
  • KCMC Medical School chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini
  • OUT (The Open University of Tanzania) ambacho ni tawi la chuo chenye jina hilohilo chenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam

Utawala

Kiutawala mji wa Moshi ni wilaya ya Mkoa wa Kilimanjaro. Ndani yake kuna kata 15 ambazo ni Bondeni, Kaloleni, Karanga, Kiboroloni, Kiusa, Korongoni, Longuo, Majengo, Mawenzi, Mji Mpya, Msaranga, Njoro, Pasua, Rau na Kilimanjaro.

Mandhari ya Moshi Mjini

Marejeo

  1. https://www.nbs.go.tz
Ramani Wilaya au manisipaa Wakazi (2022) Tarafa Kata Kijiji Eneo km²
Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro
Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro
Wilaya ya Hai 240,999 17 1,217
Wilaya ya Moshi Vijijini 535,803 32 1,300
Wilaya ya Moshi Mjini 331,733 21 63
Wilaya ya Mwanga 148,763 20 1,831
Wilaya ya Rombo 275,314 28 1,471
Wilaya ya Same 300,303 34 6,221
Wilaya ya Siha 139,019 17 1,217
Jumla 1,861,934 152 13,209
Wilaya ya Siha hii ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Hai.
Marejeo: Mkoa wa Kilimanjaro
Kata za Wilaya ya Moshi Mjini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania

Bomambuzi | Bondeni | Kaloleni | Karanga | Kiborloni | Kilimanjaro | Kiusa | Korongoni | Longuo B | Majengo | Mawenzi | Mfumuni | Miembeni | Mji Mpya | Msaranga | Ng'ambo | Njoro | Pasua | Rau | Shirimatunda | Soweto


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Moshi (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa .


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.