Knowledge Base Wiki

Search for LIMS content across all our Wiki Knowledge Bases.

Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.

Hariri viungo
Mboga sokoni
Spinachi

Mboga ni sehemu za mimea zinazopikwa na kuliwa kama chakula cha kibinadamu. Kwa kawaida tunda, jozi, mbegu au nafaka hazihesabiwi kati ya mboga.

Mifano ya mboga ni:

Chakula cha mboga chaingiza vitamini na madini muhimu katika mwili.

  • Mchicha: Majani ya mchicha yanajulikana kwa kuwa na wingi wa madini ya chuma na vitamini A na C.
  • Spinachi: Spinachi ni mboga yenye virutubisho vingi kama vile folate, vitamini K, na vitamini A.
  • Kabichi: Kabichi ni mboga inayopatikana katika aina mbalimbali, na inaweza kutumika kwa njia nyingi, ikiwa ni pamoja na kuchemsha, kukatakata, au kukaanga.
  • Broccoli: Mboga hii ina vitamini C, vitamini K, na nyuzinyuzi. Pia, imejulikana kwa kuwa na mali za kuzuia saratani.
  • Kongwe (Kale): Mboga hii inajulikana kwa kuwa na kiwango kikubwa cha vitamini K, vitamini A, na vitamini C.
  • Kitunguu Maji (Green Onions): Hii ni aina ya vitunguu vinavyotumiwa hasa kama mboga zamajani katika sahani mbalimbali.
  • Coriander (Dhania): Majani ya coriander hutumika kama viungo na pia kama mboga zamajani katika sahani mbalimbali.

*

Chakula cha kupikwa

Kwa kawaida huliwa baada ya kupikwa ingawa kuna aina zinazoliwa bichi pia kwa mfano karoti.

Mboga zamajani ni sehemu muhimu ya lishe bora na zenye afya. Matumizi yake yanaweza kuwa katika saladi, supu, sautés, na Ni njia nzuri ya kuongeza virutubisho kwenye lishe yako.

Majani mabichi

Majani mengine huliwa bichi kama ni laini sana na ladha inapendeza yanaitwa saladi. Mchanganyiko wa nyanya, vitunguu na pilipili ni kachumbari. Saladi na kachumbari huongezwa mara nyingi mafuta, chumvi na asidi ya limau au siki kwa ladha.

Mboga kama chakula cha kando

Mboga hutazamiwa kama sehemu ya chakula pamoja na ugali, ndizi au wali ambayo ni chakula cha kushibisha. Kutokana uzoefu huu wakati mwingine hata nyama huitwa "mboga" kwa maana ni chakula cha kando pamoja na ugali n.k.

Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mboga kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa .