Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.
Edmund Percival Hillary (20 Julai 1919 - 11 Januari 2008) alikuwa mpelelezi kutoka New Zealand aliyejulikana hasa kutokana na milima mingi aliyopanda.
Pamoja na sherpa Tenzing Norgay alikuwa mwanadamu wa kwanza wa kufika kwenye kilele cha Mlima Everest tarehe 29 Mei 1953.
Alijifunza kupanda milima tangu utoto wake kwao New Zealand. Alifanya kazi ya kufuga nyuki iliyomwezesha kutumia miezi ya majira ya baridi ya New Zealand kwa safari zake duniani.
Hillari alikuwa pia mtu wa kwanza aliyevuka bara la Antaktika kwa trekta.