Knowledge Base Wiki

Search for LIMS content across all our Wiki Knowledge Bases.

Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.

Hariri viungo
Jamhuri ya Benin
République du Bénin (Kifaransa)
Kaulimbiu ya taifa:
Fraternité, Justice, Travai (Kifaransa)
"Udugu, Haki, Leba"
Wimbo wa taifa: L'Aube nouvelle (Kifaransa)
"Mapambazuko mapya"
Mahali pa Benin katika Afrika ya Magharibi
Mahali pa Benin katika Afrika ya Magharibi
Ramani ya Benin
Ramani ya Benin
Mji mkuuPorto-Novo
6°29′ N 2°37′ E
Mji mkubwa nchiniCotonou
6°22′ N 2°27′ E
Lugha rasmiKifaransa
Idadi ya watu
 • Kadirio la 202314 219 908[1]


Benin, kirasmi Jamhuri ya Benin, ni nchi huru katika Afrika ya Magharibi. Awali iliitwa Dahomey.

Inapakana na Bahari ya Atlantiki upande wa Kusini, nchi ya Togo upande wa Magharibi, nchi ya Nigeria upande wa Mashariki na nchi za Burkina Faso na Niger upande wa Kaskazini.

Haihusiani na Mji wa Benin (Benin City) wala na Ufalme wa Benin wa karne ya 19.

Jiografia

Nchi ya Benin iko kati ya Mto wa Niger upande wa Kaskazini na Bahari ya Atlantiki upande wa Kusini. Haina milima mirefu.

Idadi kubwa ya watu wanaishi katika tambarare za Kusini ambapo miji mikubwa ya Benin iko, ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Porto Novo, na mji mkubwa zaidi, Cotonou. Sehemu za Kaskazini ni kavu hasa.

Nchi ya Benin inapata majira mawili ya mvua, Aprili-Julai na Septemba-Novemba. Pia kuanzia mwezi Desemba, kuna upepo ulioitwa harmattan, nao huleta vumbi na baridi wakati wa usiku.

Historia

Makala kuu: Historia ya Benin

Historia ya awali

Ufalme wa Dahomey

Sherehe na ngoma kule Abomey, 1908.

Ufalme wa Dahomey ulianzishwa katika nchi ya kisasa ya Benin.

Katika karne ya 17, ufalme huo uliotawaliwa na oba (ni cheo cha mfalme wake) ulienea sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi.

Askari wa kike wa Mfalme wa Dahomey ("Waamazoni").

Dahomey ilianzishwa na Waaja baada ya uhamisho wao kutoka Togo kuja Benin ya leo. Jina la Dahomey linasemekana kuwa limetokana na neno la Kifon la "dan" lenye maana ya "nyoka" - dokezo la ibada ya nyoka kusini mwa nchi.

Jina la mfalme wa kwanza ni Do Aklin aliyekuwa mmoja wa wana watatu wa mfalme wa Ardra waliogawanya ufalme kati yao mnamo 1625 BK. Do Aklin aliunda mji wa Abomey ukawa mji mkuu wa Dahomey.

Waaja wa Abomey walichanganyikana na wenyeji wakawa kabila jipya la Wafon au Wadahomey. Waliratibu ufalme wao kwa kuupa serikali ya mfalme mwenye nguvu, wakaunda jeshi la kudumu.

Hasa mfalme Wegbadja aliweka utaratibu kwa vizazi vilivyofuata: mfalme alikuwa mtawala mkuu, mkoani au majimboni hapana watawala wa kieneo bali watumishi wake tu.

Ardhi yote ilitazamwa kuwa mali ya mfalme mwenyewe, mafundisho yaliyohakikisha malipo ya kodi kutoka kwa wakulima waliokubali ya kwamba nchi waliyoilima ni mali ya mfalme.

Mamlaka ya mfalme yalihakikisha nguvu ya Dahomey katika mazingira yake. Jeshi la kudumu lilimpatia chombo muhimu. Ndani ya jeshi hilo kulikuwa na kikosi kimoja cha pekee ambacho kilikuwa kikosi cha wanawake.

Wasafiri wa Ulaya walikiita kikosi hiki "Waamazoni" kutokana na askari wa kike katika masimulizi ya Wagiriki wa Kale.

Wegbadja na wafuasi wake walikaza pia umuhimu wa ibada za pamoja. Wafalme wenyewe na mizimu yao walipewa nafasi muhimu. Sadaka zilienda na kila nafasi, hasa sadaka kwa mizimu ya wafalme.

Dahomey na biashara ya watumwa

Kulikuwa na utajiri mkubwa kwa sababu ya kufanya biashara na Wazungu, hasa Wareno na Waholanzi waliofika kuanzia mwisho wa karne ya 15.

Ufalme uliongezeka nguvu ya kiuchumi hasa kutokana na biashara ya watumwa. Kupaa kwa nguvu ya Dahomey kulikwenda sambamba na kuenea kwa wafanyabiashara Wazungu kwenye pwani za Afrika ya Magharibi walionunua watumwa kwa ajili ya safari ya Marekani, wakiuza silaha na bidhaa kutoka Ulaya.

Katika karne tatu za historia yake Dahomey ilikuwa kati ya wafanyabiashara wakuu wa watumwa. Pwani ya Benin ya leo ilijulikana kama Pwani ya Watumwa.

Jeshi la Dahomey lilikuwa na bunduki zilizonunuliwa kwa Wazungu wakiwauzia watumwa; silaha hizo zilitumika kwa ajili ya kupiga vita dhidi ya majirani na kujipatia wafungwa waliouzwa kama watumwa. Mapato kutoka biashara hiyo yaliwezesha wafalme wa Dahomey kununua silaha mpya.

Biashara ya watumwa iliendelea kwa karne tatu mpaka mwaka wa 1885.

Chini ya Wafaransa

Kuanzia karne ya 18, ufalme wa Dahomey ulidhoofika mpaka Ufaransa uliweza kuuvamia mwaka wa 1892. Dahomey ikawa chini ya ukoloni wa Ufaransa kuanzia mwaka wa 1899 hadi ilipopata tena uhuru tarehe 1 Agosti 1960.

Baada ya uhuru

Mpaka mwaka wa 1972 makundi mbalimbali walipigana vita, hatimaye Wakomunisti walianza kutawala chini ya kiongozi wao Mathieu Kérékou.

Hapo nchi ilipewa jina jipya, yaani Jamhuri ya Watu wa Benin, mwaka wa 1975 hadi 1991.

Tangu miaka ya 1980 nchi ilifuata mfumo wa soko huria. Kérékou alikuwa Rais hadi 1991, halafu tena miaka 1996-2006.

Katika uchaguzi wa Machi 2006, Yayi Boni alipata urais aliouanza tarehe 6 Aprili 2006.

Siasa

Makala kuu: Siasa ya Benin

Bunge la Benin lina viti 83. Huchaguliwa kila mwaka wa nne.

Rais ni mkuu wa serikali na wa nchi, naye huchaguliwa kila mwaka wa tano. Mgombea urais anatakiwa asiwe na umri wa miaka zaidi ya sabini.

Mikoa

Makala kuu: Mikoa ya Benin

Kuna mikoa 12, nayo ni:

Watu

Picha kutoka kijiji cha Benin

Kuna makabila mbalimbali ambayo watu wake wanaongea lugha tofauti sana, k.m. Kihausa, lugha za Kisonghai, lugha za Kimande na lugha za Kifula.

Kabila kubwa kabisa ni lile la Wafon (39.2%).

Lugha rasmi ni Kifaransa.

Upande wa dini, Wakristo ni 42.8% (Wakatoliki 27.1%, halafu madhehebu mengi ya Uprotestanti). Waislamu ni 24.4%. Wafuasi wa dini asilia za Kiafrika 23.3% (hasa Vodun 17.3%). Asilimia 6.5 hawana dini yoyote.

Uchumi

Uchumi wa Benin hauna nguvu sana, na hutegemea hasa kilimo, mazao ya pamba na biashara ndogondogo.

Tazama pia

Marejeo

  • Adam, Kolawolé Sikirou and Michel Boko (1983), Le Bénin. SODIMAS, Cotonou and EDICEF, Paris.

Viungo ya nje


Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Benin kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa .
  1. "Benin". The World Factbook (kwa Kiingereza) (tol. la 2024). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 23 Machi 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)