Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.
| |
Kutoka mji | London |
Nchi | Uingereza |
Eneo la utangazaji | Kote duniani |
Kituo kilianzishwa mwaka | {{{chanzo}}} |
Mwenye kituo | Shirika la umma Uingereza |
Programu zinazotolewa | {{{programu}}} |
Tovuti | www.bbc.co.uk |
British Broadcasting Corporation (BBC) ni shirika la utangazaji la Uingereza. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1922 kwa jina la British Broadcasting Company Ltd kama kampuni binafsi. Baadaye mwaka 1927 lilibadilishwa hadhi yake na kuwa shirika la umma.
BBC ndio shirika la habari kubwa kuliko yote duniani likiwa linatoa habari na taarifa mbalimbali kwa njia ya redio, runinga na intaneti.
Tangu mwaka 1957 imerusha habari kwa Kiswahili pia.
Kwa mujibu wa BBC, lengo lake ni kutoa habari, kuelimisha, na kuburudisha. Kauli mbiu yake ni "Nation Shall Speak Peace Unto Nation", kwa kiswahili ikimaanisha " Taifa itasema amani kwa Taifa".
Shirika hili linaongozwa na Bodi ya Magavana wanaochaguliwa na Malkia au Mfalme wa Uingereza kwa ushauri toka kwa mawaziri wa serikali ya Uingereza. Hata hivyo, BBC inasema katika katiba yake kuwa inafanya kazi zake bila shinikizo toka kwa wanasiasa au wafanyabiashara na kuwa linawajibika kwa wasikilizaji na watazamaji wake tu.
Matangazo kwa lugha ya Kiswahili yalianza mwaka 1957. Tarehe 27 Juni 1957 sauti ya Kiswahili ilisikika mara ya kwanza; msemaji alikuwa Oscar Kambona aliyekuwa wakati ule mwanafunzi wa chuo kikuu huko London na baadaye waziri wa mambo ya nje wa kwanza baada ya uhuru wa Tanzania.[1]
Idhaa ya Kiswahili ya BBC imepanuka huduma zake hadi televisheni na intaneti. Tangu 2014 imehamisha ofisi na programu zake zote kuja Afrika ya Mashariki, ikirekodi Dar es Salaam na Nairobi.