Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.
Waraka wa tatu wa Yohane ni kimojawapo kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Kuhusu mwandishi wa barua hiyo lilichelewa kutajwa jina la Mtume Yohane kutokana na yaliyomo na mtindo wa uandishi wake.
Kama mwandishi si yeye, ni mmoja wa wanafunzi wake aliyeandikwa mwishoni mwa karne ya 1 huko Efeso.
Mlengwa ni Gaio, anayedhaniwa kuwa kiongozi mmojawapo wa jumuia fulani kati ya zile zilizomtegemea Yohane.