Infrastructure tools to support an effective radiation oncology learning health system
Yaliyomo
Bundesliga ni jina linalotumika katika michezo mbalimbali huko Ujerumani na Austria. Mpira wa miguu ni mchezo mashuhuri sana katika nchi hizo mbili. Na ndiyo maana mchezo wa mpira wa miguu unajulikana sana katika nchi hizo kwa jina la Bundesliga.
Timu za mpira zinaingia katika Bundesliga kwa kuwa washindi katika moja kati ya ligi ndogo za nchini humo. Timu itakayoongoza katika msimu wa mashindano hayo inaitwa Meister. Meister ni neno la Kijerumani lenye maana ya bingwa au mshindi. Kisheria, msimu wa michezo ya mpira huwa na kawaida ya kuanza Juni katika mwaka uliopo hadi Juni mwaka unaofuatia. Timu itakayoongoza itategemea na ushindi au pointi walizozipata wakati wa msimu huo. Msimu huo umegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni mzunguko wa kwanza na mzunguko wa pili.
Vilabu hamsini na sita vimefanikiwa kushiriki katika ligi hiyo ya Bundesliga tangu kuanzishwa kwake. Bayern Munich imeshinda kombe hilo mara 31. Hata hivyo Bundesliga imekua na mabingwa wengine kama Borussia Dortmund, Hamburger SV, Werder Bremen, Borussia Mönchengladbach, na VfB Stuttgart maarufu zaidi miongoni mwao. Bundesliga ni moja ya ligi kubwa kitaifa zilizoshika nafasi ya nne barani Ulaya kulingana na kiwango cha ubora katika ligi ya UEFA kwa msimu wa 2021-2022. Wachezaji wake wamekusanya tuzo tisa za Ballon d'Or, tuzo mbili za mchezaji bora wa FIFA, Viatu vinne vya dhahabu Ulaya, na tuzo tatu za mchezaji wa mwaka wa UEFA kwa wanaume ikiwa ni pamoja na Mchezaji bora wa Mwaka katika mashindano ya UEFA klabu.[1][2]
Bundesliga ni ligi ya soka namba moja duniani kwa wastani wa mashabiki 45,134 kwa kila mchezo wakati wa msimu wa 2011-12 Bundesliga hutangazwa kwenye televisheni katika nchi zaidi ya 200. Bundesliga ilianzishwa mwaka 1962 katika mji wa Dortmund na msimu wa kwanza ulianza mwaka 1963-64. muundo na shirika la Bundesliga, pamoja na ligi nyingine za soka za Ujerumani, zimefanyika mabadiliko ya mara kwa mara. Bundesliga ilianzishwa na Ujerumani Fußball-Bund. Shirikisho la Soka la Ujerumani), lakini kwa sasa inaendeshwa na Deutsche Fußball Liga.
Klabu
Klabu | Nafasi katika msimamo wa ligi msimu wa 2021–22 | Msimu wa kwanza kucheza Bundesliga | Idadi ya misimu aliyocheza Bundesliga | Msimu wa kwanza katika ligi ya Bundesliga | Idadi ya misimu aliyocheza bila kushuka daraja | idadi ya makombe ya ligi ya Bundesliga aliyochukua | Ubingwa kimataifa | Kombe la ligi la mwisho kuchukua |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
FC Augsburgb | 14th | 2011–12 | 12 | 2011–12 | 12 | 0 | 0 | – |
Bayer Leverkusenb | 3rd | 1979–80 | 44 | 1979–80 | 44 | 0 | 0 | – |
Bayern Munichb | 1st | 1965–66 | 58 | 1965–66 | 58 | 31 | 32 | 2022 |
VfL Bochum | 13th | 1971–72 | 36 | 2021–22 | 2 | 0 | 0 | – |
Borussia Dortmunda | 2nd | 1963–64 | 56 | 1976–77 | 47 | 5 | 8 | 2012 |
Borussia Mönchengladbach | 10th | 1965–66 | 55 | 2008–09 | 15 | 5 | 5 | 1977 |
Eintracht Frankfurta | 11th | 1963–64 | 54 | 2012–13 | 11 | 0 | 1 | 1959 |
SC Freiburg | 6th | 1993–94 | 23 | 2016–17 | 7 | 0 | 0 | – |
Hertha BSCa | 16th | 1963–64 | 39 | 2013–14 | 10 | 0 | 2 | 1931 |
1899 Hoffenheimb | 9th | 2008–09 | 15 | 2008–09 | 15 | 0 | 0 | – |
1. FC Kölna | 7th | 1963–64 | 51 | 2019–20 | 4 | 2 | 3 | 1978 |
RB Leipzigb | 4th | 2016–17 | 7 | 2016–17 | 7 | 0 | 0 | – |
Mainz 05 | 8th | 2004–05 | 17 | 2009–10 | 14 | 0 | 0 | – |
Schalke 04a | 1st (2. B) | 1963–64 | 54 | 2022–23 | 1 | 0 | 7 | 1958 |
VfB Stuttgarta | 15th | 1963–64 | 56 | 2020–21 | 3 | 3 | 5 | 2007 |
Union Berlinb | 5th | 2019–20 | 4 | 2019–20 | 4 | 0 | 0 | – |
Werder Bremena | 2nd (2. B) | 1963–64 | 58 | 2022–23 | 1 | 4 | 4 | 2004 |
VfL Wolfsburgb | 12th | 1997–98 | 26 | 1997–98 | 26 | 1 | 1 | 2009 |
a = Mojawapo ya timu zilizo anzisha ligi ya bundesliga
b = Timu ambayo haijawahi kushuka daraja katika ligi kuu tangu ilipoanzishwa
Timu zilizopo katika msimamo wa ligi kuu ya bundesliga 2022/2023
Uwezo wa klabu
Mnamo mwaka 2004, heshima ya ujio wa "Verdiente Meistervereine" ilianzishwa kufuatia desturi ya kwanza kufanyika nchini Italia kutambua pande ambazo zimeshinda michuano mitatu au zaidi tangu 1963 kwa kuonyesho nyota za dhahabu kwenye beji(nembo) za jezi za timu zao. Matumizi ya kila nchi ni ya kipekee, na sheria zifuatazo zinatumika nchini Ujerumani:
- 3 Bundesliga titles: 1 star
- 5 Bundesliga titles: 2 stars
- 10 Bundesliga titles: 3 stars
- 20 Bundesliga titles: 4 stars
- 30 Bundesliga titles: 5 stars
Idadi ya makombe ya ligi
- Bayern Munich (31)
- Borussia Dortmund (5)
- Borussia Mönchengladbach (5)
- Werder Bremen (4)
- Hamburger SV (3)
- VfB Stuttgart (3)
Klabu | Washindi | Mshindi wa pili kwenye ligi | Bingwa wa ligi | Misimu aliyoshinda nafasi ya pili kwenye ligi |
---|---|---|---|---|
Bayern Munich | 31 | 10 | 1968–69, 1971–72, 1972–73, 1973–74, 1979–80, 1980–81, 1984–85, 1985–86, 1986–87, 1988–89, 1989–90, 1993–94, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2004–05, 2005–06, 2007–08, 2009–10, 2012–13, 2013–14, 2014–15, 2015–16, 2016–17, 2017–18, 2018–19, 2019–20, 2020–21, 2021–22 | 1969–70, 1970–71, 1987–88, 1990–91, 1992–93, 1995–95, 1997–98, 2003–04, 2008–09, 2011–12 |
Borussia Dortmund | 5 | 8 | 1994–95, 1995–96, 2001–02, 2010–11, 2011–12 | 1965–66, 1991–92, 2012–13, 2013–14, 2015–16, 2018–19, 2019–20, 2021–22 |
Borussia Mönchengladbach | 5 | 2 | 1969–70, 1970–71, 1974–75, 1975–76, 1976–77 | 1973–74, 1977–78 |
Werder Bremen | 4 | 7 | 1964–65, 1987–88, 1992–93, 2003–04 | 1967–68, 1982–83, 1984–85, 1985–86, 1994–95, 2005–06, 2007–08 |
Hamburger SV | 3 | 5 | 1978–79, 1981–82, 1982–83 | 1975–76, 1979–80, 1980–81, 1983–84, 1986–87 |
VfB Stuttgart | 3 | 2 | 1983–84, 1991–92, 2006–07 | 1978–79, 2002–03 |
1. FC Köln | 2 | 5 | 1963–64, 1977–78 | 1964–65, 1972–73, 1981–82, 1988–89, 1989–90 |
1. FC Kaiserslautern | 2 | 1 | 1990–91, 1997–98 | 1993–94 |
1860 Munich | 1 | 1 | 1965–66 | 1966–67 |
VfL Wolfsburg | 1 | 1 | 2008–09 | 2014–15 |
Eintracht Braunschweig | 1 | 1966–67 | ||
1. FC Nürnberg | 1 | 1967–68 | ||
Schalke 04 | — | 7 | 1971–72, 1976–77, 2000–01, 2004–05, 2006–07, 2009–10, 2017–18 | |
Bayer Leverkusen | — | 5 | 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2001–02, 2010–11 | |
RB Leipzig | — | 2 | 2016–17, 2020–21 | |
Meidericher SV | — | 1 | 1963–64 | |
Alemannia Aachen | — | 1 | 1968–69 | |
Hertha BSC | — | 1 | 1974–75 |
Viungo vya nje
- Map to all Germany clubs
- Official site Ilihifadhiwa 6 Aprili 2007 kwenye Wayback Machine. (Kiingereza)
- DFB — Deutscher Fußball Bund (German Football Association)
- Kicker.de (Kijerumani)
- Federal league archives (Kijerumani)
- News and features from the Bundesliga presented by the Deutsche Welle (in seven languages, including English and German)
- News about Bundesliga (Kijerumani)
- All-time statistics (Kiingereza)
- German Bundesliga match previews Ilihifadhiwa 12 Juni 2008 kwenye Wayback Machine. (Kiingereza)
- Bundesliga Table Ilihifadhiwa 21 Mei 2008 kwenye Wayback Machine. (Kiingereza)
Marejeo
- ↑ Cutler, Matt (15 Juni 2010). "Bundesliga attendance reigns supreme despite decrease". Sport Business. Iliwekwa mnamo 4 Januari 2012.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "TV BROADCASTERS WORLDWIDE". Retrieved on 2022-07-29. Archived from the original on 2013-05-20.
- ↑ 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 3.10 3.11 3.12 3.13 3.14 "Capacity German Bundesliga stadiums 2020/21". Statista.
- ↑ "Dortmunder Stadion wird ausgebaut" (kwa Kijerumani). Sport1. 16 Julai 2015. Iliwekwa mnamo 17 Julai 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Stadiums in Germany". World stadiums. World stadiums. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 8 Septemba 2018.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Verein". dierotenbullen.com (kwa Kijerumani). Leipzig: RasenballSport Leipzig GmbH. n.d. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Juni 2016. Iliwekwa mnamo 12 Mei 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)