Infrastructure tools to support an effective radiation oncology learning health system
Yaliyomo
Mandhari
Tarehe 1 Desemba ni siku ya 335 ya mwaka (ya 336 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 30.
Matukio
- 1640 - Mfalme Yohane IV wa Ureno anamaliza kipindi cha maungano ya kifalme kati ya Ureno na Hispania; Ureno unakuwa nchi huru tena
Waliozaliwa
- 1925 - Martin Rodbell, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1994
- 1951 - Jaco Pastorius, mwanamuziki kutoka Marekani
- 1973 - Lombardo Boyar, mwigizaji wa filamu kutoka Marekani
- 1981 - Khamis Mussa, mwigizaji na mwanamuziki kutoka Tanzania
- 1982 - Diego Cavalieri, mchezaji mpira kutoka Brazil
Waliofariki
- 1433 - Go-Komatsu, mfalme mkuu wa Japani (1392-1412)
- 1521 - Papa Leo X
- 2007 - Elisabeth Eybers, mwandishi wa Afrika Kusini
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu nabii Nahumu, Kastrisiani, Florensa, Leonsi wa Frejus, Donolo wa Le Mans, Ajeriki, Eliji wa Noyon, Edmundi Campion, Rudolf Sherwin, Aleksanda Briant, Charles de Foucauld n.k.