Trends in LIMS
Yaliyomo
Mandhari
Tarehe 9 Mei ni siku ya 129 ya mwaka (ya 130 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 236.
Matukio
- 1945 - Ujerumani unasaini mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia katika Ulaya.
Waliozaliwa
- 1921 - Mona Van Duyn, mshairi kutoka Marekani
- 1927 - Manfred Eigen, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1967
- 1936 - Ernest Shonekan, Rais wa Nigeria (1993)
- 1938 - Charles Simic, mshairi kutoka Marekani
- 1947 - Michael Levitt, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 2013
- 1950 - Jorie Graham, mshairi kutoka Marekani
- 1953 - Bernard Kamilius Membe, mwanasiasa wa Tanzania
- 1955 - Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa Ethiopia
- 1957 - Beatus Kinyaiya, askofu Mkatoliki nchini Tanzania
- 1970 - Ghostface Killah, mwanamuziki kutoka Marekani
- 1972 - AZ, mwanamuziki kutoka Marekani
Waliofariki
- 1760 - Nikolaus von Zinzendorf, askofu wa Kanisa la Moravian nchini Ujerumani
- 1931 - Albert Abraham Michelson, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1907
- 1968 - George Dillon, mshairi kutoka Marekani
- 1986 - Tenzing Norgay, mpelelezi kutoka Nepal
Sikukuu
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Nabii Isaya, Herma wa Roma, Pakomi, Wafiadini mia tatu na kumi wa Uajemi, Denisi wa Vienne, Geronsi wa Cervia, Beatus wa Vendome, Yosefu Do Quang Hien n.k.