Knowledge Base Wiki

Search for LIMS content across all our Wiki Knowledge Bases.

Type a search term to find related articles by LIMS subject matter experts gathered from the most trusted and dynamic collaboration tools in the laboratory informatics industry.

Mahali pa Spitsbergen
Spitzbergen kutoka satelaiti wakati wa joto (mwezi wa Julai: peupe ni barafu)

Spitsbergen (pia: Spitzbergen) ni kisiwa kikubwa cha funguvisiwa la Svalbard linaloitwa mara nyingi kwa jina la Spitsbergen vilevile kwa jumla. Kiko ndani ya Bahari ya Aktiki na eneo lake ni km² 39,044. Funguvisiwa lote ni sehemu ya ufalme wa Norwei.

Mwinuko mkuu ni mlima wa Newtontoppen wenye kimo cha mita 1717.

Wakazi wa kisiwa ni Wanorwei na Warusi: kwa jumla hawazidi watu 2100.

Biashara ya kisiwa ni utalii na migodi pekee; hakuna kilimo kutokana na baridi. Mimea hustawi katika wiki chache za joto kidogo na hii inatokea kwenye asilimia 10 ya eneo la kisiwa pekee, maeneo mengine ni baridi mno.

Kuna kijiji kimoja ambacho ni Longyearbyen wenye wakazi 1700. Cha pili ni Barentszburg kinachokaliwa na Warusi 400 wanaozidi kupungua. Pyramiden ilikuwa kituo kikubwa cha kuchimba makaa lakini haina watu tena tangu mwaka 2000.

Historia

Spitsbergen haina wenyeji asilia. Visiwa vilitembelewa na wavuvi tu waliowinda nyangumi wengi. Tangu karne ya 18 walikuwepo wawindaji wachache waliojenga vibanda na kukaa hapa kwa muda wa miaka lakini hapakuwa na wakazi wa kudumu kabisa.

Mnamo mwaka 1900 makaa yaligunduliwa kwa wingi na sasa makazi ya kwanza ya kudumu kwa ajili ya wafanyakazi yalijengwa. Kwa njia hii Longyearbyen ilianzishwa mwaka 1906. Hadi wakati ule hakuna nchi iliyokuwa na mamlaka juu ya visiwa.

Mnamo 1920 nchi za Norwei, Denmark, Ufaransa, Italia, Japani, Uswidi, Marekani na Ufalme wa Maungano (Uingereza) zilikubaliana masharti ya mkataba wa Spitsbergen. Masharti mawili muhimu ni ya kwamba

  1. funguvisiwa litakuwa chini ya mamlaka ya Norwei
  2. nchi zote zinazotia sahihi kwenye mkataba huo zina haki ya kuwa na shughuli za kiuchumi kwenye visiwa.

Nchi nyingine zilijiunganisha na mkataba baadaye. Lakini ni Norwei na Urusi pekee ambazo zina shughuli kwenye visiwa hivi. Wakati wa Umoja wa Kisovyeti walikuwepo Warusi wengi waliochimba makaa na madini mengine lakini migodi yote haileti faida tena, imefungwa kwa kiasi kikubwa.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Norwei bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Spitsbergen kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa .